
TUNAWEZAJE KUTUNZA AFYA YA AKILI ZETU KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU?
Kwa kutojihusisha na matukio yoyote yenye ushawishi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kusababisha kuzorota au udhaifu kwa afya zetu za akili au kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wake
Mambo hayo ya kusaidia kutunza afya zetu za akili ni kama vile kuwa na mitazamo chanya (mzuri) juu yako mwenyewe na maisha yako binafsi, maendeleo yako, na watu au vitu vinavyotuzunguka, ushirikiano, kujitawala, mtazamo kuhusu hali halisi ya maisha na kumudu mazingira yanayokuzunguka ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na watu, lakini pia kujenga mahusiano yenye nguvu na mazingira hayo.
Afya ya akili ni dhana inayoweza kutazamwa kijamii na kutafsiriwa namna tofauti katika jamii tofauti,makundi,tamaduni,taasisi na wataaluma mbali mbali. Wote hao wana njia tofauti ya kueleza asili, sababu, ustawi au uhalisia wa afya ya akili na utekelezaji unaofaa katika kuitunza au kutibu.
Kwahiyo, kutokana kwamba Afya ya Akili inategemeana na mtazamo wa jamii, wataalamu ya Afya ya akili, hutibu matatizo au magonjwa ya akili kulingana na mtazamo wa mtu kutoka jamii husika. Mfano, wengine hulinganisha muhusika/ muadhilika na mazingira yake kama vile tamaduni yake, kipato chake, hitikadi za kisiasa, kidini, na kijamii kwa ujumla wake. Kwa kufuata mtazamo huo inamsadia mtaalamu kuchagua njia sahihi ya kutibu magonjwa ya akili
Magonjwa ya akili au kwa kingereza, mental disorders/mental illnesses or psychiatric disorders, yanaweza kuangaliwa katika namna ya tabia na akili. Magonjwa ya akili husababisha, dhiki, kuzorota au udhaifu kwa akili na mwili kufanya kazi ipasavyo.
Dhiki, kuzorota au udhaifu huo vinaweza kujitokeza mara moja au kwa mwendelezo au kujirudia rudia kulingana na aina ya ugonjwa hudika.
Magonjwa mengi ya akili yanajidhiihirisha kwa dalili au ishara mbalimbali zinazofanana au kutofautiana kulingana na ugonjwa mmoja na mwingine.
Mara nyingi magonjwa ya akili au dalili zake huonekana kulingana na mwenendo au tabia ya mtu inavyoanza kubadilika, jinsi anavyowaza na jinsi anavyojisikia au mtazamo wake unavyoanza kubadilika. Pia, mawazo yake hutoka chanya na kuwa hasi katika maisha yake ya kila siku.
Pamoja na hayo, wataalam wa Afya ya akili wanapotaka kutambua (diagnosis) ugonjwa husika wa akili lazima wazingatie tamaduni, hitikadi za dini,siasa, uchumi, imani, kanuni na taratibu za jamii husika.
Hii ni kwasababu, ugonjwa flani wa akili katika jamii moja unaweza usionekane kama ni ugonjwa katika jamii nyingine kulingana na mazoea, mtazamo na tamaduni ya jamii husika.
Mwaka, 2013, taasisi kubwa ya kisaikolojia ya kimarekani “the American Psychiatric Association (APA) katika DSM-5, ilitoa maana ya magonjwa ya akili kwamba ni dalili au hali inayoambatana na usumbufu mkubwa na udhaifu ambapo mtu hushindwa kuleta usawa au uwiano wa utambuzi wa hisia au tabia na na akili kushindwa kufanya kazi kisaikolojia, kibailojia na kijamii. Visababishi vya magonjwa ya akili hutofautiana kulingana na gonjwa hudika na mtu mwenyewe na mazingira yanayomzunguka