Opening: Monday to Saturday
Call Us: +255 742 501 501 or +255 683 551 117
e-mail: info@mht.care

Nini Maana ya Afya ya Akili #AfyaYaAkili

October 27, 2019 MHT Admin No Comments

Nini Maana ya Afya ya Akili #AfyaYaAkili

Afya ya akili ni nini?

Ni hali ya kuwa sawa kiakili na kisaikolojia au kutokuwepo kabisa kwa usumbufu wa akili ya mtu, mfano msongo wa mawazo.

Ni hali ya kuwa na mawazo chanya, kuwa sawa kijamii na kisaikolojia na kuweza kuchangia katika utendaji wako wa kila siku na uwezo wa kuridhisha wa kimawazo na kitabia.

Huhusisha uwezo wa mtu kufurahia maisha na kutengeneza mlingano baina ya shughuli zako kimaisha pamoja na jitihada zako kufikia uwiano mzuri kisaikolojia, kutoka kwenye msongo utokanao na magonjwa, misiba na shida mbali mbali.

Pia ni uwezo wa mtu kuishi katika mabadilko mbalimbali ya kimaisha na kufanyia kazi changamoto mbalimbali kimaisha.

Uwezo wa mtu kuwa timamu kiakili huhusisha mtu kuwez kutatua matatizo mbalimbal yanayomkabili yahusishayo msongo wa mawazo katika maisha, shuguli za uzalishaji na mchango wa mtu husika katika jamii.

Afya ya akili huhusisha…..”ustawi wa akili, kujitambua kwa ufanisi, uhuru, umahiri, utegemezi wa ulimwengu, na kujitambua kwa uwezo wa kiakili na kihemko, kati ya wengine.”

Ustawi wa mtu ni uwezo, kukabiliana na mikazo ya kawaida ya maisha, kazi yenye tija na mchango kwa jamii yao.

Tofauti za kitamaduni, tathmini ya kujifanya, na nadharia za kitaalam zinazoshindana zote zinaathiri jinsi mtu anafafanua “afya ya akili”.

Watu wenye afya bora ya akili wanaweza pia kuwa na magonjwa ya akili, na watu ambao hawana ugonjwa wa akili pia wanaweza kuwa na afya mbaya ya kiakili.

Leave a Reply

Translate »