Klabu za afya ya akili Tanzania

Klabu za afya ya akili Tanzania,Ni miongoni mwa program zinazolenga kutoa elimu ya ujuzi na uelewa juu ya afya ya akili kwa wadau stahiki

Walengwa hapa ni wadau tofauti wakiwemo vijana walio na wasio katika mfumo wa elimu ,kama vile shule,vyuo ,vyuo vya kati na vikuu,vyuo vya ufundi  pamoja na wale wa mtaani.

VIPI UTAANZISHAJE KLABU?

Mtu yeyote anaweza kuanzisha klabu hii, kama tu atakuwa na nia ya dhati kujisaidia na kuwasaidia wengine juu ya changamoto mbalimbali za afya ya akili na hasa katika kutoa elimu na jinsi ya kukabili changamoto za kisaikolojia na afya ya akili kwa ujumla.

Idadi ya wanachama wa kuanzia ni watano(5),ambao baada ya kujiunga watachagua viongozi wao akiwemo mwenyekiti,katibu na mratibu wa klabu. Wanachama watalazimika kuandaa katiba ya klabu itakayotumika kama muongozo kwa wanachama na kufuata mwongozo wa taasisi kupitia programu ya mental Health Forum, chini ya kiongozi wake Mratibu wa Klabu za Afya ya Akili Taifa (Mental Health Clubs Tanzania)

SHUGHULI ZA KLABU

Klabu hii mara tu itakapoanzishwa katika taasisi,italazimika kuwa na shughuli ambazo zinalenga kuwaleta pamoja wanachama wake,kwa kukutana mara kwa moja, kama vile ,mara moja kwa wiki ,kwa mwezi nakadharika kadiri wanachama watakavyoona.

Miongoni mwa shughuli mnazoweza kufanya ni pamoja na :-

  • Wanachama baada ya kuanzisha,Watalazimika kutambua kuwa,Klabu ya Mental Health Tanzania,Ni jukwaa linalotoa wigo wa kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu afya aya akili kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
  • Wanachama watajadili kuhusu taarifa toka vyanzo tofauti zenye mnasaba wa matukio yanayohusu afya ya akili.
  • Watasaidiana kupitia viongozi walio na mafunzo maalum,Kushauriana na wao kwa wao,pamoja na kwa msaada wa kuwabaini na kuwasaidia wenye uhitaji walio nje ya klabu.
  • Ni sehemu ya kwanza ya furaha ,ponyo na faraja kwa kila mwanachama.
  • Wanaklabu wataandaa  na kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka juu ya taasisi ya Mental Health Tanzania,pamoja na shughuli inazofanya.
  • Watalazimika kuheshimiana,kuthaminiana na kulindana heshima zao kila mmoja.
  • Kujadili juu ya elimu ya awali ya afya ya akili .
  • Kutoa muda wa kuwasikiliza wenye uhitaji wa kusikilizwa kwa yale yanayowasumbua katika fikra.
  • Kuzielewa changamoto za matatizo ya kiakili kwa majina na dalili zake.
  • Kuwa na mijadala inayolenga kuzitambua na kutafuta changamoto za afya ya akili na kujua mbinu sahihi za kuwasaidia wenye nazo katika mazingira yanayowazunguka wanachama.
  • Kila mwanachama atakuwa ni balozi wa Mental Health Tanzania,Hivyo atalazimika kufahamu majukumu ya msingi ya taasisi na  kuwa tayari kuitangaza popote atakapokuwa.
  • Wanachama watalazimika kuwa na eneo maalum la kukutania,kama bustanini,darasani,na mfano wake,ambalo litafahamika kama  MHT CAMP.
  • Wanachama watachagua mwalimu mlezi ,Ambae wanampenda na kumuamini,ambae atawasaidia  katika kufuatilia na kukamilisha shughuli za klabu ndani na nje ya klabu. Wanachama watapendekeza jina la mwalimu na Mratibu taifa atamwandikia barua ya kumuomba kuwa mlezi wa klabu hiyo.
  • Klabu italazimika kuandaa ripoti ya nini inafanya katika shughuli zake za msingi kila baada ya miezi mitatu na kuituma makao makuu ya Mental Health Tanzania kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.

NINI KLABU ITAPATA KUTOKA MENTAL HEALTH TANZANIA?

Ili kuwa na ufanisi katika klabu zetu, Mental Health Tanzania itatoa ushirikiano kama ifuatavyo;

  • Usajili wa klabu  utakaotoa namba maalum  itakayotumika kama uthibitisho wa kutambuliwa.
  • Mafunzo ya mara ya kwanza kwa viongozi na wanachama wote wa klabu  itakayosajiliwa  kuhusu afya ya akili.
  • Mafunzo ya mara kwa mara ya viongozi na wanachama katika ofisi zetu pindi watakapohitaji kutoka mental health Tanzania.
  • Kutoa viongozi na wataalam ambao watashiriki pamoja katika shughuli za klabu na matukio ya Klabu.
  • Kuwaunganisha viongozi na wanachama katika makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii kama  Whatsapp,Telegram na mfano wake,Ili kurahisisha utoaji wa taarifa.
  • Kutoa  vipeperushi  na makala tofauti zenye elimu ya afya ya akili.
  • Kuwaunganisha  na watalaam zaidi wa afya ya akili kwa wanachama watakaokuwa na changamoto za afya ya akili.

MUONGOZO WA UENDESHAJI WA KLABU YA AFYA YA    AKILI CHINI YA TAASISI YA MENTAL HEALTH TANZANIA

UTANGULIZI:

Klabu ya Mental   Health Tanzania, Ni miongoni mwa programu zinazolenga kutoa elimu ya ujuzi na uelewa juu ya afya ya akili kwa wadau stahiki.

Walengwa hapa ni wadau tofauti wakiwemo vijana walio na wasio katika mfumo wa elimu  ,kama vile shule ,vyuo , vyuo vikuu na vyuo vya kati ,ufundi pamoja na wale walio mtaani.

Ili klabu kupanga na kutimiza malengo iliyojiwekea,kutakuwa na uongozi utakaotokana na kuchaguliwa au kuteuliwa na wanachama wenyewe.

MAMBO YANAYOKAMILISHA USAJILI WA KLABU

  1. Kikundi cha vijana cha zaidi ya watu watano watakao unda klabu.
  2. Jina la klabu
  3. Viongozi wa kikundi
  4. Mlezi-Kiongozi
  5. Shughuli za klabu
  6. Katiba ya klabu
  7. Sajili klabu yenu katika taasisi ya Mental Health Tanzania
  8. Tuma taarifa kwa taasisi kila baada ya miezi mitatu kupitia email address

UONGOZI WA KLABU

Uongozi utachaguliwa na wanachama wenyewe mara tu baada ya kuanzishwa klabu na kupokea  nambari ya usajili maalum kutoka Mental Health Tanzania.

Kutakuwa na nafasi tano za uongozi kama zifuatazo ,Mwenyekiti, Katibu,  Afisa wa fikira zetu, (wawili-Msichana na Mvulana) na Afisa mawasiliano. Nafasi nyinginie ni ya mlezi wa Klabu.

MAJUKUMU YA VIONGOZI

Mwenyekiti – Huyu  ndio kiongozi mkuu wa Klabu shuleni au kwenye taasisi husika.

  • Atachaguliwa na wanachama kupitia utaratibu wa kutajwa jina na kupigiwa kura.
  • Atafungua  na kuongoza vikao vya wanachama pia shughuli nyingine za klabu.
  • Atakuwa miongoni mwa wawakilishi wa klabu katika mafunzo na shughuli mbalimbali.
  • Ni balozi wa kwanza wa Mental Health Tanzania, na atasimama na kuitangaza popote atakapokuwa.
  • Atalazimika kuripoti kwa mratibu wa klabu taifa  kupitia ripoti maalum ya kila mwezi ,itakayokuwa ikionesha kazi zinazofanywa na klabu yake.
  • Atapanga na kuratibu shughuli mbalimbali zinazopaswa kufanywa na klabu yake.

Katibu – Ni mtendaji mkuu wa shughuli za klabu za kila siku.

  • Ataitisha na kuwaalika wanachama katika vikao na shughuli za Klabu.
  • Atahusika na kuandika muhtasari wa vikao na shughuli za wanachama.
  • Ataandika ripoti za shughuli na vikao mbalimbali vya klabu itakayoidhinishwa na mwenyekiti wake.
  • Atakuwa miongoni mwa wawakilishi wa klabu katika mafunzo na shughuli mbalimbali.
  • Ni balozi wa kwanza Mental Health Tanzania, na atasimama na kuitangaza popote atakapokuwa.
  • Ni msimamizi mkuu wa nidhamu katika shughuli  katika klabu.

Emotional Supporter (Afisa wa fikira zetu) – Huyu  ni mshauri wa kwanza wa wanachama wa klabu.

  • Kupitia mafunzo maalum, Emotional Supporter atahusika na kumtambua  mtu mwenye uhitaji wa kusaidiwa kisaikolojia.
  • Atakuwa na fursa ya kumsikiliza na kisha kumuongoza mwenye uhitaji kwa mtu au idara itakayompa msaada mfano ,kuwasiliana na mratibu wa klabu kwa ajili ya kumuunganisha mteja huyo na mtaalam kwa mwanasaikolojia au mtaalamu mwingine wa afya ya akili.
  • Nafasi hii itakuwa na watu wawili ,Mmoja kutoka upande wa  wavulana na mwingine upande wa wasichana.

Afisa Mawasiliano – Ni mtu mwenye jukumu la kuandaa na kusambaza taarifa mbalimbali ndani na nje ya Klabu.

  • Atakuwa na jukumu la kuandaa kumbukumbu za matukio yote ya shughuli za klabu kupitia njia ya picha za mnato na mjongeo (Still and Video).
  • Atalazimika kufuatilia kwa karibu taarifa zinazoendelea katika jamii inayomzunguka zenye mlengo wa afya ya akili, kuziandaa na kuziwasilisha kwa wanachama na taasisi aliyopo kwa ujumla.
  • Ana jukumu la kuendeleza mahusiano baina ya wanachama wa klabu nyingine katika shule au taasisi yake,pamoja na zile zilizo nje ya taasisi aliyopo.
  • Atawakilisha klabu yake katika shughuli mbalimbali zitakazolenga kuzungumza juu ya wanayofanya.Kama kwenye Redio,TV na mitandaoni.
  • Huyu ndie msemaji mkuu wa shughuli za klabu na yanayoendelea baada ya taarifa kuidhinishwa na mwenyekiti wake.
  • Atalazimika kuendesha akaunti za mitandao ya kijamii ya klabu yake.

MLEZI – Huyu ni mshauri mkuu wa wanachama wa klabu, ambaye atapatikana kwa kupendekezwa na wajumbe wenyewe kisha kuidhinishwa na Mental health Tanzania kwa kupata barua rasmi.

Majukumu yake

  • Kuratibu shughuli zote za klabu ndani na nje ya eneo ilipo.
  • Kuidhinisha na kusimamia rufaa za wanachama watakaoonekana kuhitaji msaada zaidi wa kisaikolojia.
  • Kusimamia malengo ya klabu kutokana na taratibu na mipango iliyojiwekea.
  • Atakuwa ndio msimamizi wa nidhamu za wanachama kwa kuwashauri na kuwalekezea pale inapohitajika.

SIFA ZA   JUMLA ZA KIONGOZI

  • Awe tayari kuongoza
  • Awe msiri
  • Awe tayari kujifunza
  • Mwenye moyo wa kusaidia wengine.
  • Awe na heshima
  • Apende watu kama anavyopenda kupendwa yeye.

JINA LA KLABU

Mara baada ya kuamua kuanzisha klabu katika eneo mtakalopenda iwepo,Wanachama watalazimika kuchagua jina lenye kuenenda na shughuli wanayofanya,Ambalo mwisho litamalizia na neon MHT Club.

Mfano,Mwanza Sekondari MHT Club.

Ni lazima jina liwe na maana nzuri linaloendana na maudhui ya afya ya akili.

KATIBA YA KLABU

Ndio muongozo wa namna gani mtaendesha shughuli zenu kila siku.

Katiba ioneshe jina lenu,shughuli mnazofanya,Nani ni nani na yapi majukumu yake,Utaratibu wa kusaidiana kimasomo na mfano wake,Na mengine yote yatakayoonekana yana umuhimu kufanywa na wachama kadiri mtakavyoona.

SAJILI KLAB YENU KATIKA TAASISI MENTAL HEALTH TANZANIA

Ni lazima ili kuendelea na shughuli zenu mpate Baraka zote za usajili wa klabu yenu kwa kutuma fomu maalum itakayoidhinishwa na Mental Health Tanzania kwa kupewa namba maalum ya usajili.

Sajili kwa kutuma taarifa zenu zinazoonesha jina la klabu na mahali mlipo kwenda nambari 0655  08 02 90 , Usiache pia kutuma nakala ya katiba yenu kwa Mental Health Tanzania,Sanduku la posta ni  218 ,Mwanza,Tanzania. Tutawatumia cheti na barua ya kuwafahamisha kwamba sasa mmesajiliwa kama klab ya MHT.

TUMA RIPOTI

Ili tujue nini mnafanya, Ni lazima mtume taarifa ya ripoti  kila baada ya miezi mitatu kwa mratibu wa Klabu za mental health Tanzania.

Ripoti ikusanye mambo haya,Jina la klab,sehemu mlipo,idadi ya wanachama ,tarehe ilipoanzishwa,Idadi ya mikutano mliyofanya,Changamoto,fursa na mafanikio,Taarifa nyingine ambazo mtapenda kutushirikisha.

Tunawatakia kila la heri katika shughuli zenu za klabu

MAWASILIANO:

Ili kuendelea kuwa karibu na Mental Health Tanzania,usiache kuwasiliana na uongozi  na msimamizi wa idara ya Klabu ya  Mental health Tanzania ,Brother Hilal Magege kupitia nambari 0655 0802 90

“Mental Health TanzaniaWellbeing of the Mind”

FOMU YA USAJILI WA KLABU YA MENTAL HEALTH TANZANIA

Tafadhari jaza fomu hii kama tu tayari umekwishasoma na kuuelewa muongozo wa klabu za Mental Health Tanzania.

A: SEHEMU HII IJAZWE NA VIONGOZI WA KLAB PEKEE

 1. JINA LA KLABU………………………………………………………………………………………………..
 2. NAMBA YA USAJILI WA KLABU…………………………………………………………………………….
 3. MAHALI ILIPO ………………………………………………………………………..
 4. VIONGOZI WA KLABU (Majina, nafasi ya uongozi na Mawasiliano yao)
 • ……………………………………………………………………………………………………………….
 • ………………………………………………………………………………………………………….
 • ……………………………………………………………………………………………….
 • ………………………………………………………………………………………………………
 • ……………………………………………………………………………………………
 • ………………………………………………………………………………………………………
 1. KAULI MBIU YA KLABU…………………………………………………………………………….
 2. JINA LA MRATIBU ………………………………………………………………………………………
 3. IDADI YA WANACHAMA …………………………………………………………………..
 4. TAREHE YA KUANZISHWAKLABU………………………………………………..

B: SEHEMU HII IJAZWE NA UONGOZI WA ENEO ILIPO KLABU PEKEE

Klabu hii imethibitishwa kuanzishwa, na uongozi wa eneo hili utakuwa tayari kushirikiana na uongozi wa klabu na mlezi katika kufafanikisha matukio mbalimbali yenye kuwasaidia vijana wetu kufahamu juu ya afya ya akili.

JINA……………………………………………………………………………………………

NAFASI ………………………………………………………………………………………

SAHIHI……………………………..TAREHE…………………………………

 

C: KWA MATUMIZI YA OFISI PEKEE

KLAB HII IMETHIBITISHWA LEO …………………………………………NA KUPEWA NAMBARI YA USAJILI: ……………………………………………………………….

SAHIHI YA MRATIBU WA KLAB TAIFA……………………………………….

MAWASILIANO: BARUA PEPE –   ,S.L. P 218, Mwanza, Tanzania

Simu: 0655 08 02 90 (WhatsApp pia)