
KAMA UNAONA UNADHARAULIWA FANYA YAFUATAYO NDANI YA SIKU 7 UTAPEWA HESHIMA POPOTE
Karibu kila mmoja wetu amepitia mapito ya kutolewa kauli zenye kuchochea hasira kutoka kwa watu mbalimbali
Hivyo kitendo cha kulea maumivu ndani kwa ndani si kizuri na kuwajibu vibaya wenye kukusema kwa lugha mbaya ni kupoteza muda
Kwa watu wengi 90% hutumia njia hizi Aggressive Behavour, Passive Behavior na Ukitumia njia hizi utazidi kuteseka siku zote
Jinsi ya kukabiliana na kila aina ya mtu ukionana nae ni rahisi endapo utaamua kubadilika
Njia ambazo hazifai ni
1.AGGRESSIVE BEHAVIOR
Hapa utakuta labda mzazi,mlezi,mtu aliekusomesha,mwajiri wako,ndugu zako au wadogo zako , marafiki zako au majirani wanakufanyia vitendo vyenye kuchochea hasira
Vitendo kama kukujibu kwa mkato,kukuzomea, kukufokea, kukutukana, kukosoa kwa lugha mbaya, kejeli, lawama, vijembe,
ukiongea wanacheka sana kwa sauti ya juu,kukuaibisha kwa makusudi,
Kutoa maoni kwa kauli mbaya
Kukuita majina mabaya,utani wenye maudhi,kukupa vitisho,kulaani, kusambaza umbea,vitendo vyenye utovu wa nidhamu
Katika hali hii utaona muonekano wa sura zao na maumbile yakiwa hivi
SAUTI
sauti ya juu sana,sauti yenye ukali na hasira, kukatiza kauli zako ,matusi, lawama, kukosolewa kwa ukali.
MUONEKANO WA SURA NA MAUMBILE
Utaona uso wenye hasira,mishipa imesimama,meno yamekaza,macho yenye kulengwa na machozi
Kunyooshewa kidole