Visababishi vya ugonjwa wa Skizofrenia-1

Tafiti hazijabainisha sababu moja ya skizofrenia. Inafikiriwa kuwa mwingiliano kati ya vinasaba na sababu mbalimbali za kimazingira zinaweza kusababisha skizofrenia.

Vinasaba vina mchango mkubwa katika kubainisha hatari ya kutokea kwa Skizophrenia, japokuwa watu wengi ambao wamegundulika na ugonjwa huu hawana historia ya kuwa naugonjwa huu katika familia.

Ujauzito na matatizo pindi mama anapojifungua huku kukiwa na upungufu katika usambazaji wa oksijeni kwenye tishu za mwili na umri mkubwa wa mzazi (greater paternal age) vina uhusiano mkubwa na hatari ya kupata Skizophrenia kwa mtoto aliezaliwa (developing fetus).

Kwa kuongezea, matatizo mengine wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua, kama vile msongo wa mawazo, maambukizi, upungufu wa lishe, ugonjwa wa kisukari kwa mama, na matatizo mengine ya afya, yameunganishwa na kwenye hatari ya mtoto atakae zaliwa kua na Skizophrenia

Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba wengi wa watoto walio na viashiria hivi vya hatari hawapati ugonjwa wa Skizophrenia. Mambo haya yote yanachangia kwenye kundi la sababu za kisababishi ambazo zinaathiri kuanza kwa ugonjwa huo.

Leave a comment

6 + 16 =