Ugonjwa wa wasiwasi wa kijamii (SOCIAL ANXIETY DISORDER)

Imeandaliwa na:
Onesmo Maganga (Mwanasaikolojia). Simu: 0757961389

Umewahi kuona mtu hawezi kuongea mbele za watu?

Anatetemeka, anaogopa, haendi kwenye sherehe au mikusanyiko umewahi kujiuliza shida n nini?

Umewahi kujiuliza kwanini mtu hawezi kabisaa kukaa mbele darasani?

Umeshawahi kujiuliza kwanini mtu anachelewa kuoa au kuanzisha mahusiano au familia na muda tayari* na *pengine ameptiliza?

Nimewaletea baadhi ya majibu Kisaikolojia, simaanishi hii ndio sababu pekee ila Ina weza kuwa sababu ya baadhi ya maswali hayo na mengine Mengi.

Tunaposema Social Anxiety: ni pale ambapo mtu anakua na wasiwasi akiwa Kati ya watu wengi anao wafahamu au asio wafahamu au pale ambapo mtu anapaswa kufanya Jambo mbele ya watu wengi. Anakua na hisia hasi ndani mwake juu ya mtazamo wa watu wengine juu yake.

Anaweza akahisi Kama hayuko vizuri, au hafanyi uwasilishaji/ presentation Nzuri au anahisi muonekano wake hauko vizur anajishuku nk.

Wasiwasi huu anaweza kuoneshwa katika hali au matukio yafuatayo.

 1. Kuepuka mazungumzo au kukutana na watu asiowafahamu katika matukio ya kijamii. Mfano, anaweza asiende kabisaa au akaenda akaondoka mapemaa au akiwepo akakosa utulivu kabsaa.
 2. Anaweza kushindwa kula au kunywa, kucheza mbele ya wengine au kutoa hotuba au kula kiapo mbele za watu. Utotoni :

Hii inaonekana katika mazingira rika au peer group. Watu wa rika lake, anakua anawasiwasi akiwa nao na wakati mwingine hachezi nao kabisa, anajisikia salama akiwa na watu wazima.

Mtoto wasiwasi unapozidi, huonyeshwa kwa kulia, hasira, kung’ang’ana na kushindwa kuzungumza katika hali za kijamii.

Wasiwasi huu ukiendelea kwa miezi sita na kuendelea huitwa ugonjwa na mtu huyu huhitaji msaada wa Kisaikolojia au Counseling. Hapa simaanishi kwamba Ni lazima itokee utotoni inaweza kutokea ukubwani pia kulingana na Mambo unayoyapitia.

VIASHIRIA VYA TATIZO HILI:

 1. Je, una hofu kubwa au wasiwasi katika hali za kijamii au matukio ya kijamii? Unahisi kuchunguzwa chunguzwa au Kuwa na wasiwasi kwamba unaonekanaje unapokua katika matukio ya kijamii?
 2. Je, unajisikia, kuogopa, kufadhaika, kuonekana mjinga,kuudhi wengine au kuboa, kudharaiwa, au wasiwasi wakuonekana tofauti na wengine hasa katika matukio ya kijamii?
 3. Mtu mwenye wasiwasi huu wakati mwingine hutetemeka mikono anapokua katika mazingira ya watu wengi au matukio ya kijamii, anaweza kuepuka kunywa, kula au kunyosha kidole hadharani ndo wale mkitoka darasani anasema jibu la swali aliloulizwa mwalimu baada ya Mwalimu kutoka, ambapo wote mlishindwa na mkapigwa akiwemo na yeye, baadaye anasema jibu ni hili analaumiwa kwanini hakusema kumbe pengine anashida hii.
 4. Katika mazingira haya mtu anaweza kutokwa jasho jingi, watu hawa huepuka kupeana mikono au kula chakula chenye viungo vingi, kuogopa ,kuona haya usoni, kuepuka maonyesho ya hadharani, mwanga mkali Hawa wataomba uzime taa kidogo au uweke taa za rangi hawapendi kuonekana nk.

5.Shy Bladder syndrome au paruresis:
hofu ya kuogopa kukojoa kwenye choo cha umma wakati mtu au watu wengine wapo…maana yake Ni kwamba Kama ukumbini Kuna vyoo mtu huyu hawezi kwenda kwenye vyoo vya humo ndani ataenda nje au mbali sana, anaogopa kuwa watu wanaweza kuwa wanamzungumzia au Wana mchunguza.

Madhara ya ugonjwa huu ni:

 1. Mtu anashindwa kuhudhuria karamu au sherehe Kama ni mwanafunzi inawezekana akaepuka kwenda shule.
 2. Anakosa uthubutu na anakua na unyenyekevu kupita kiasi ambao ni shida pia anakua ndio kwa kila kitu.
 3. Mtu huyu anaaibu na wakati mwingine anaogopa kutazamana na mtu, yaani kukutanisha macho.

4.kuzungumza kwa sauti nyororo au ya chini kupita kiasi, pia anakosa uwezo wa kuanzisha mazungumzo, hapa kutongoza ni shida .

 1. Hutafuta kazi ambayo haitaji kukutana Sana na watu, wengi hupenda kazi za kwenye mitambo, computer na nyingine zisizohusisha watu wengi au mikusanyiko, huyu hawezi kuwa Mc au Cameraman.
 2. watu hawa wanaweza kukaa nyumbani kwa muda mrefu, kuchelewa kuoa na kuwa na familia.

  Usisahau ku share na wengine wanufaike na machache hayo. Asante.

Leave a comment

4 × 3 =