Wagonjwa wa afya ya akili waongezeka

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema katika kipindi cha July, 2023 hadi March 2024 waliohudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa shida ya magonjwa ya afya ya akili
walikuwa 293,952 sawa na 6.3% ya wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza ikilinganishwa na 246,544 sawa na 6% kwa kipindi cha mwaka 2022/23.

“Wagonjwa waliolazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya wenye magonjwa ya afya ya Akili walikuwa 19,506 sawa na 7% ya wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza ikilinganishwa na wagonjwa 13,262 sawa na 5% katika kipindi cha mwaka 2022/23, ongezeko hili la wagonjwa 116 wa afya ya akili limetokana na kuongezeka kwa uelewa wa jamii kuhusu magonjwa haya na kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma”

MillardAyoUPDATES

Leave a comment

1 × two =