Visababishi vya magonjwa ya akili

Magonjwa ya akili na changamoto za kisaikolojia yanaweza kutokea kwa mtu yeyote na mda wowote, kwa watu wa kila kizazi, rangi, dini, tabaka na rika lolote katika jamii.

Kuna sabababu tofauti tofauti za magonjwa ya akili ambayo uharibu mfumo mzima wa mtu kwa namna ya kutenda, kifikiri na kuhisi. Sababu hizo ni kama vile za kisaikolojia, kibaioloji na za kimazingira.

Mfano; Visabaishi vya kimazingira vya magonjwa ya akili na changamoto za kisaikolojia, huletwa na mambo mengi yameendekea kutokea hapa duniani na ktk maisha yetu ya kila siku, misongo ya mawazo tunayoishi nayo, ukatili wa kijinsia, unyanyapaa, uraibu wa madawa, migogoro ya ndoa na familia, changamoto kazini, masomoni, uchumi, malezi ya watoto, n.k

Takribani watu bilioni 1 wanaishi na magonjwa ya akili duniani, mtu 1 kati ya watu wazima 8 atapitia hali ngumu ya afya ya akili au kupata magonjwa ya akili katika maisha huku mahala pa kazi mtu 1 kati ya watu 5 huwa na matatizo ya afya ya akili.

Leave a comment

1 × 3 =