Magonjwa ya akili ni nini?

Ni matokeo ya mabadiliko ya ufanyaji kazi wa ubongo kutokana na mwingiliano wa vinasaba na mazingira ya mtu.

Mabadiliko haya uhathiri au kuingilia utendaji kazi wa mtu wa akili (impairing his/her functioning) katika kufikiri, kuhisia na matendo/tabia.

Kama ilivyo kwa magonjwa ya mwili kuwa mengi, ndivyo ilivyo kuna magonjwa mengi ya akili. Kila ugonjwa wa akili una dalili zake na aina ya matibabu yake.

Dalili za ugonjwa wa akili zinaweza kuwa za kimwili, kihisia au kiakili. Dalili za magonjwa ya akili au mtu kuwa au kutokuwa na afya nzuri ya akili, kutaonekana katika nyanja kuu tatu ambazo ni: (1) Fikra/mawazo (2) Hisia/mihemko (3) Tabia au matendo.

Hivo dalili za magonjwa ya akili ni kwamba utaanza kuona/ kuhisi au kuwa na hali ambayo isio ya kawaida/tofauti (Deviant). Hali hiyo sio ya kufurahisha inachukiza inakuletea shida, uzuni, msongo, inakuhudhi au kubugudhi (Distress). Na hiyo hali inaingiliana na kazi zako za kila siku (Dysfunction). Mpaka hapo utajua hii inaweza kuwa changamoto ya afya ya akili. Dalili za moja kwa moja za ugonjwa husika zitaanza kujitokeza katika kipindi husika.

Mfano kama ni sonona (depression) utaanza kuwa na dalili angalau 5 kati ya dalili nyingi za sonona kwa mfululizo wa wiki 2 tu karibu kila siku inatosha kukufanyia utambuzi (diagnosis) wa sonona. Mfano, dalili za ugonjwa wa akili mmojawapo unaoitwa sonona (Depression) ni kama vile

Kukosa usingizi; Kukosa hamu ya kula; Kuchoka kupita kiasi (unyogovu); Kujitenga na watu; Kushindwa kushiriki katika shughuli ambazo hapo awali zilikuwa zikikufurahisha na unazipenda; Kupoteza umakini; Kutingwa na mawazo; Kutawaliwa na mawazo ya kufa au kujitoa uhai na hata kujaribu kufanya hivyo; Kulia mara kwa mara; Kukata tamaa ya maisha; Kuwa na maumivu endelevu ya sehemu mbali mbali za mwili kama vile kichwa, mgongo, n.k kusahau kulikopita kiasi na kukumbuka mambo hasi zaidi na kuyapa uzito.

Leave a comment

twelve − 3 =