Imani potofu kuhusu magonjwa ya akili

Jamii inaaminishwa na  zimejengeka imani  potofu kwamba magojwa ya akili yanasababishwa na uchawi, imani za kidini, imani za kitamaduni kama vile kuamini kwamba mgonjwa wa akili ni matokeo ya kutolewa kafara, ni laana, bahati mbaya, na adhabu za mizimu, au Mungu na miungu.

Hali hii hupelekea wagonjwa wa akili kutafuta matibabu kutoka kwa watabibu wa jadi, viongozi wa kidini au waanga wa magonjwa ya akili kubaki bila kutibiwa milele.

Kwa sababu ya imani potofu, unyanyapaa na ubaguzi, watu wengi wanateseka na wanashindwa kufikia malengo yao ya maisha au kutafuta huduma za afya ya akili.

Leave a comment

fifteen + 2 =