Afya ya Akili ni nini?

Ni hali ya ustawi wa kisaikolojia na kijamii. Ustawi huu wa afya  ya akili unahusisha  tunavyofikiria, tunavyohisi na tunavyotenda. Ni hali ya mtu kutambua uwezo alionao, anaweza kuendana na msongo wa kawaida wa maisha, na ana uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji na kuchangia katika jamii yake.


Ili mtu awe na afya nzuri ya akili (ustawi), tunategemea kisaikolojia na kijamii, awe na fikra chanya ( mawazo yake yawe ni ya ustawi mzuri)

Hisia zake na mihemuko iwe chanya. Matendo yake yawe chanya. Anajitambua na kujielewa uwezo wake na anaweza kudhihilisha huo uwezo kwa fikra, hisia na matendo. Anaweza kuzalisha (productive).

Muhimu zaidi ni pale hayo yote yanaweza kufanyika hata kama kuna changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku; yaani bila kujali misongo ya mawazo ya kawaida ya kila siku tunategemea fikra, hisia na matendo, kujitambua na kuzalisha viwe chanya.
Ikiwa ni kinyume cha maelezo hayo, basi mtu huyo anaweza kuwa na changamoto ya afya ya akili au ugonjwa wa akili.

Leave a comment

nine − 9 =